Header Ads Widget

WEKA TANGAZO LAKO HAPA 0626883962

USIPOTUMIA ELIMU YAKO KUENDESHA MAISHA YAKO,ELIMU HIYO ITATUMIWA NA WATU WENGINE KUENDESHA MAISHA YAO

 UJASIRIAMALI NI UTAJIRI

  • MWANDISHI
  • JUSTINE MISIGARO

Kwa kuanza niwasalimu ndugu wapenzi wa blog Yetu Pendwa,bila Shaka Mnajifunza na kuburudika kwa kuperuzi ndani ya Blog yenu Pendwa.

1...Leo ndugu wapendwa nimependa nizungumze juu ya Hali ya Uchumi na maendeleo ya mtu binafsi. 

Dunia tuliyonayo sasa ni ya sayansi na teknolojia,Kiufupi Matumizi ya Nguvu katika kutimiza majukumu mbali mbali yamepungua kama sio kuisha kabisa.

Ili kujikwamua kiuchumi Kila mtu amekuwa na Njia mbali mbali ilimradi tu kujipatia kipato na kuendesha Maisha. 

Nimeshuhudia Idadi Kubwa ya Vijana wakiwa mtaani baada ya kuhitimu Shule na Vyuo na kutumia muda mwingi Kulalamikia Serikali kwa habari ya kutopewa ajira Hali ya kuwa tayari wana taaluma ambazo zingeweza kuwasaidia kuwa wabunifu katika kutumia Mazingira wanayoishi kutengeneza Pesa. 

Kama Wahenga wasemavyo kuwa Elimu ni Ufunguo wa Maisha na sio Ufunguo wa Ajira! 

Zipo fursa nyingi ambazo kijana mwenzangu ukiamua kuacha kutumia Bando lako kuangalia Comedy na filam mitandaoni unaweza Kuzifanya kwa mtaji mdogo na ukavuna Pesa pasipo kuajiriwa. 

Kijana mwenzangu ukumbuke kuwa Nchi yetu bado inaendelea kukua na haina viwanda vya kutosha ajira kwa wahitimu maelfu wanaohitimu kila mwaka na wala Serikali haina uwezo wa kuajiri watu wote wanaohitimu shule,vyuo vya Kati na vya juu Kwa wakati mmoja. 

Nitumie wino huu kukufumbua macho ili uzione fursa zinazokuzunguka hapo hapo ulipo kwenye mazingira yako.

Chukua mfano mzuri,Vijana tumekuwa na kasumba ya kuchagua kazi za kufanya Baada ya kuhitimu na kusahau kuwa tumetokea katika mazingira ya familia duni za Mpini na Jembe,Tukitoka Jembe tunajiona Sisi sio wa kilimo wala ufugaji Bali ni wa kukaa kwenye kiyoyozi na Viti vya kuzunguka"HAPO NDIPO SHIDA INAPOANZIA*

Kusudi la Serikali kukusomesha ni pamoja na wewe kutumia Elimu hiyo kuisaidia Serikali katika Kubuni miradi endelevu ambayo itawezesha Serikali kupata Kodi na Kodi hizo kurudi kukusaidia wewe mwenyewe katika Mahitaji ya kijamii ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya Afya,Barabara na Uchumi. 

Utakuta mtu ahitimu eg. Degree ya Kilimo na Mifugo,Ufugaji wa nyuki,Uhandisi wa majengo,Udaktari na Mengineyo kama hayo lakini bado analalamika Ajira serikalini Hali ya kuwa Taari ameshapewa Skills ambazo ni Ajira tosha.

Niishukuru Serikali kwamba Miaka ya karibuni imeleta mikopo nafuu kwa vijana na makundi mbali mbali ya ujasiriamali,Lakini hata hivyo vijana wengi tunashinda mitandaoni kuperuzi yasiyo ya msingi na kushindwa kufata taratibu kwa namna gani tunaweza kupata hyo mikopo nafuu inayotolewa serikali kwa Makundi mbali mbali.

Imani yangu ni kwamba kila mhitimu wa Shule,Chuo cha Kati na cha juu anao uwezo tayari wa kufanya jambo akawa mfano hata kwa wale ambao wako Shule au vyuoni kuliko kukaa mtandaoni kulalamika tu bila kuchukua hatua.

  • IKIWA UTASHINDWA KUTUMIA ELIMU YAKO KUENDESHA MAISHA YAKO, ELIMU HIYO ITATUMIWA NA WENGINE KUENDESHA MAISHA YAO

  1. IMEANDALIWA NA:
  2.  Justine Misigaro
  3. MOBILE:0713 292 508


Post a Comment

0 Comments