Header Ads Widget

WEKA TANGAZO LAKO HAPA 0626883962

CHOZI LA SAMAKI

MWANAUME MASHINE

 *NOTE*

Wanaume wengi Hawavai vizuri si kwa sababu hawapendi fashion,

Bali maisha yamewavalisha majukumu hadi wamesahau hata kujinunulia shati jipya.


Wanakaa kimya, hawalalamiki

Kwa sababu walishajifunza kuwa machozi yao siyo habari, bali mzigo wa kuchekwa.


Huyu mwanaume unayemuita 'mbwa'  ndiye anayesambaza chakula kwa familia nzima.

Anakopa,anajinyima, anakataliwa,lakini bado anaendelea kupambana – kimya kimya.


Asubuhi kabla ya jua kuchomoza,ameondoka. Usiku akiwa amechoka anarudi.

Hajui kulalamika, hajui kuomba huruma,lakini moyo wake umebeba dunia nzima.


Wanawake,si kila kimya ni uzembe...

Wengine kimya chao kimejengwa na uchungu wa kupuuziwa na mliotakiwa kuwa mabega yao.


👉 Waheshimu wanaume wa kweli  wanaotunza hata kwa maumivu.

👉 Wanapopotea kidogo siyo kwa mapenzi ni kwa shinikizo la maisha.💯✍


       *By*

*Justine Misigaro*

Post a Comment

0 Comments