Header Ads Widget

WEKA TANGAZO LAKO HAPA 0626883962

Historia ya Wilaya ya Kibondo

 MWANDISHI
Justine F Misigaro
0713292508

            

             PORI LA AKIBA MOYOWOSI

UTANGULIZI

Wilaya ya kibondo ni moja Kati ya Wilaya za Mkoa wa Kigoma,Wilaya hii iko umbali wa Kilomita 270 Kaskazini ya Makao Makuu ya Mkoa wa Kigoma. 

Kibondo ilitangazwa rasmi kuwa Wilaya Mwaka 1954.

Wilaya hii ina jumla ya kata 19,Ilipofika Mwaka 2012 iligawanywa na kupatikana Wilaya nyingine ya Kakonko. 

Wakazi wa Wilaya hii ni kabila la Wahambwe(Waha). 

Jumla

Mkoa wa Kigoma una jumla ya Wilaya zipatazo saba,Wakazi wa Mkoa huo ni kabila la waha. 

Maelezo

Waha wamegawanyika katika makundi yapatayo Mawili au Matatu. 

  • >Wahambwe
  • >Wanyaheru
  • >Wayungu

Wahambwe

Hawa Wanapatikana katika wilaya ya Kibondo

Wanyaheru

Hawa Wanapatikana katika wilaya ya Kasulu na Wilaya ya Buhigwe

Wayungu

Wayungu Wanapatikana Katika Wilaya ya Kakonko. 

Hawa Wayungu,Wahambwe na Wanyaheru wote kwa ujumla wao wanaitwa Waha,Pamoja na tofauti zao zinazotokana na Mahali wanapotokea lakini haiwafanyi kuona kama kuna tofauti kati Yao kwa kuwa wote ni Wazawa Wa Mkoa Wa Kigoma na Lugha yao ni Kiha japokuwa kuna tofauti katika baadhi ya maneno wakati Wa kuongea Lugha ya Kiha. 

Aisha Waha Wa Kasulu,Kigoma mjini na vijijini pia Waha Wa Buhigwe wanaelewana zaidi wanapoongea Kiha kuliko wanapoongea na waha Wa kibondo,Vivyo hivyo Waha Wa Kibondo wanatofautiana katika kuongea Kiha na Waha Wa Kakonko japokuwa Lugha ni moja hiyo hiyo ya Kiha,Pamoja na hayo lugha hiyo haiwafanyi washindwe kuelewana Katika mazungumzo kwa kuwa asilimia kubwa ya maneno ni yaleyale tofauti yake ni Matumshi na baadhi ya maneno machache hususani Majina ya Vitu. 

SHUGHURI ZA KIUCHUMI

Wakazi Wa Kibondo hujishughulisha zaidi na Kilimo cha jembe la Mkono na mazao yanayolimwa zaidi ni Mahindi,Karanga,Maharage,Mbaazi na Mihogo,Japokuwa kwa siku za karibuni Kilimo cha Mhogo kimewavutia wengi baada ya Kuonekana kama zao la kibiashara baada ya Wafanyabiashara kutoka nchi jirani za Congo,Burundi na Rwanda kuonesha uhitaji mkubwa Wa zao hilo,Kilimo cha Mhogo kimekuwa mkombozi kwa wakazi Wa Wilaya ya Kibondo na kuwawezesha kuendesha Maisha Yao kwa uhakika kwani wengi kutokana na Biashara hii wamefanikiwa kujenga Nyumba za kisasa,Wamenunua vyombo vya moto(Pikipiki na Magari) Na wengine wamepata mitaji ya Kufanya Biashara mbadala. 

UTAMADUNI

Kama ilivyo kwa Mikoa mingine na Wilaya zingine,Wilaya ya Kibondo inazo tamaduni zake ambazo zinawafanya Watu kuishi kwa umoja na Amani,Wakazi Wa Kibondo wana ngoma za Asili ambazo hupigwa kipindi cha sherehe za kitaifa na wakati mwingine hupigwa kipindi cha Sherehe za Harusi za Kimila,Ngoma hizo ni UMUYEBHE na AGASIMBO,Chakula kikuu wilayani Kibondo ni Ugali na Maharage,Japokuwa kutokana na mabadiriko ya kiutamuduni,Kisayansi na teknolojia kwa sasa hakuna Chakula rasmi cha Asili kwa kuwa Wanakula vyakula vya aina mbali mbali. 

Wilaya ya Kibondo upande Wa magharibi imepakana na miji Kadhaa ya nchi jirani ya Burundi ambayo ni KAYOGORO, KISULU NA CHANKUZO. 

Kibondo Ni wilaya ambayo imejaaliwa Uoto Wa Asili hivyo kusaidia kuwa na vyanzo vingi vya maji,Ukifika Kibondo utagundua kuwa ni Mahali ambapo pana jiografia nzuri kwa ajili ya Ufugaji na Kilimo cha Umwagiliaji,Pia wakazi Wa Kibondo ni Wakarimu wanapenda Wageni.

Yako mengi ya kujifunza na kujivunia hususani unapotembelea Wilaya ya Kibondo na Mkoa Wa Kigoma kwa Ujumla kwa kuwa kuna Vivutio pia vya kitalii kama vile,Pori la akiba la Moyowosi,Fukwe za ziwa Tanganyika Na hifadhi zingine nyingi za wanyama pori zinazopatikana katika Mkoa Wa Kigoma bila kusahau Hifadhi ya Gombe ambapo utajionea Sokwe Wa ajabu ambao hujawahi kuwaona popote,Tembelea Kibondo,Tembelea Mkoa Wa Kigoma ujionee utofauti na Sehemu zingine. 


Post a Comment

0 Comments